Na Shushu Joel, Mkuranga.
MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu ametoa vyerehani 28 kwa ajili ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika kila kata na vitatu vitabaki Wilayani kwa lengo la kukuza uchumi wa viongozi wa jumuiya hiyo.
![]() |
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vyerehani hivyo Mhe Mgalu alisema kuwa amegawa vyerehani Mkoa mzima lengo likiwa ni kuwainua wanawake wa Mkoa wa Pwani kiuchumi ili waweze kujiongezea kipato mmoja mmoja.
Aidha amewataka wale wote waliofanikiwa kupata vyerehani hivyo kuhakikisha wanavitumia kama vile ilivyokusudiwa ili waweze kupiga hatua ya kiuchumi.
Akizungumza na wale wote waliokabidhiwa vyerehani hivyo Mwenyekiti wa UWT Taifa Mery Chatanda amemshukuru Mhe Mgalu kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitoa ili kusaidia jumuiya hiyo.
Aidha amewataka Wanawake wengine kuiga kile ambacho kimekuwa kikifanywa na Mhe Mgalu kwani amekuwa kielelezo cha mafanikio ya Jumuiya kwa ujumla.
MWISHO
0 Comments