MNEC GHULAM AWAONYA WACHONGANISHI


Na Shushu Joel, Mkuranga 


MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  anayetokana na Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Bi Nadra Ghulam amewakumbusha  wananchi wa kata ya Shungubweni Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kutokusikiliza maneno ya uongo yanayoenezwa na wapinzani.


Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na umati wa wananchi uliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo.


Aidha Mnec Nadra Ghulam amesisitiza kuwa ni vyema kuwapuuza wale wote wanaobeza maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kitu ambacho ni aibu sana kwani wananchi ni mashuhuda wakubwa kwa kile kinachofanywa na Rais wetu. 


"Mwaka huu kuendelea katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ni lazima wana ccm tujitokeze kwa wingi ili tukamuheshimishe Rais Dkt Samia " Alisema Mnec Nadra Ghulam 


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mbezi Wilayani Mkuranga Rashid Serungwi amempongeza Mnec Nadra kwa kutatua kero za papo kwa papo jambo ambalo limekiongezea kura nyingine chama cha Mapinduzi. 


Aidha amemuomba kuendelea kuwa na moyo huo wa kupenda wanqnchi hakika Mnec ni kiongozi wa kuigwa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments