"WANAO MKEJELI RAIS SAMIA HAWAJITAMBUI" MNEC NADRA GHULAM


Na Shushu Joel, Chalinze


MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa anayetokana na Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Nadra Ghulam amewataka wananchi wa Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani kupuuza maneno yanayotolewa na watu wasiojielewa juu ya maneno ya kumkejeli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.


Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata Mbwewe mara baada ya ukaguzi wa miradi ya elimu, Afya na Umeme ambayo kwa asilimia kubwa inaendelezwa na kukamilishwa na Rais Dkt Samia kwa kiwango cha hali ya juu.


Aidha amewataka wananchi kutokusikiliza wachumia tumbo ambao wameshindwa la kukosoa na badala yake wameanza kumkejeli Rais wetu jambo ambalo limekosa mashiko kwa wananchi.


"Wananchi wenzangu msikubali kutenganishwa na Chama chenu cha Mapinduzi nyie endeleeni kushirikiana nacho kwani maendeleo yanayofanywa na Dkt Samia mnayaona" Alisema Mnec Nadra Ghulam 


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo Diwani Ndugu Omary Abas alisema kuwa wameipongeza jumuiya ya umoja wa Wanawake Tanzania kwa kufanya ziara katika kata hiyo na kujionea miradi mbalimbali inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Aidha aliongeza kuwa wao kama wananchi wanaona kejeli wanazomfanyia Rais wetu hivyo amemwakikishia Mnec Ghulam kuwa katika kata ya Mbwewe hakuna kura ya Dkt Samia itakayopotea .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments