Na Shushu Joel
MJUMBE wa Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Taifa na Mbaraza wa Jumuiya hiyo Hajat Mariam Ulega amewataka watu wenye nafasi kujitoa kwa jamii isiyojiweza ili Mungu aweze kuwaongezea.
Rai hiyo ameitoa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kinachoelekea ukingoni ambapo amejitolea tani moja ya Michele,tani moja ya sukali na mafuta ya kupikia ndoo kumi kwa ajili ya watoto wenye uhitaji.
"Siku zote unapojitoa kwa wenzako Mungu ubariki jambo hilo na kukuongezea pale unapopatoa" Alisema Hajat Mariam Ulega.
Aidha alisema kuwa hakuna binadamu aliyekuja hapa duniani kwa bahati sote tumekuja kwa mpango wa Mungu hivyo hata Mungu wetu anafurahishwa sana nasi pale anapotuona tunasqidia viumbe vyake alivyoviumba.
Pia amewataka watanzania kila mmoja kwa imani yake kuendelea kuliombea Taifa letu ili amani tuliyonayo iendelee kudumu kizazi na kizani.
MWISHO
0 Comments